SWAHILVERSION: WE DEM BOIZ REMIX VIDEO

0 comments
http://image1.spreadshirtmedia.com/image-server/v1/compositions/1001512380/views/1,width=235,height=235,appearanceId=2/WE-DEM-BOYZ.jpg
Soma Zaidi»

T.I AKANA KASHFA YA WIZI WA BEAT

0 comments


BAADA ya huku kupita kwa mtayarishaji wa muziki Pharrell na msanii Robin Thicke kulipa dola milioni 7.3 kwa familia ya Marvin Gaye sasa kibao kimemgeukia Rapa T.I. kwa madai kuwa inasemekana na yeye ni miongoni wa wasanii wanaoiba mawazo ya watu.

Hali hiyo imeibuka mara baada ya  kulipwa dola milioni $7.3 kutoka kwa producer Pharrell na msanii Robin Thicke, Familia ya Marvin Gaye sasa imeanza kumhughulikia rapa T.I ambaye pia ameweka sauti kwenye wimbo wa “Blurred Lines”.

T.I Ameulizwa na Tmz kuhusu kesi hii nakujibu ” Sijui kinachoendelea, sihusiki na hio kesi kabisa na mimi napenda sana kazi za Marvin Gaye, ila nawakubali sana Pharrell na Robin, Mimi ni mwandishi, mbunifu, siibi mawazo ya watu, na mtu yeyote mwenye akili ataona hilo”

Soma Zaidi»

HIZI NDIZO HABARI ZA KWELI KUHUSU UVUMI WA KIFO CHA VENGU

0 comments
BADO hali ya uvumi katika mitandao ya kijamii inaendelea huku kuvumishwa kwa vifo kwa baadhi ya wasanii, ambapo hivi karibuni imezuka story ambayo imeenea sana mitandao ya kijamii na pia watu wamekuwa.

 wakitumiana PICHA Whatsapp na wengine wameweka pia kwenye kurasa za Instagram na kuandika #RIP inayomuonesha picha ya mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Joseph Shamba aka Vengu ambaye ni muda mrefu hajaonekana akiigiza pamoja na kundi lake baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Seki ambaye ndiye muongozaji wa kundi hilo amekanusha kwa taarifa hzo na kudai kuwa ni taarifa za uongo ambazo zimeenezwa na watu wazushi.

Wakizungumza na Clouds FM muda mfupi uliopita Seki pamoja na Joti wameeleza wazi kuwa hakuna ukweli wowote juu ya taarifa hizo.
MSAFARA wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam siku ya alhamis, kabla ya kuunganisha ndege siku ya ijumaa kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili. Katika msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi amewajumuisha wachezaji nane (8) katika kikosi chake wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe. Wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ni Limbikani Mzava (Celtic), Harry Nyirenda (Black Leopards), Esau Kanyenda (Polokwane City), na Atusaye Nyondo (University of Pretoria). Wengine ni Nahodha Joseph Kamwendo (Tp Mazembe - Congo DR), Frank Banda (HBC Songo - Msumbuji), Chimango Kayira (Costal De Sol - Msumbuji) na Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe).

Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt

Soma Zaidi»

Nay wa Mitego Amfumania Mchumba Wake Siwema Kitandani na Kiserengeti Boy

0 comments
KABAANG! Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, amedaiwa kumfumania ‘laivu’ mchumba wake Siwema akiwa kitandani na ‘serengeti boy’ wake ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, Ijumaa lina full stori.

NI MWANZA
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mwanzo mwisho, tukio hilo lilichukua nafasi Machi 15, mwaka huu maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza ambako mrembo huyo alikuwa akiishi, baada ya Nay kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa mrembo huyo usiku wa Machi 14 alionekana akiponda raha ndani ya klabu moja iliyopo katika jengo la Hoteli ya Golden Crest.

“Wambeya walimpenyezea habari Nay, kesho yake asubuhi sana akatimba Mwanza kwa ndenge na kumkuta laivu Siwema akiwa na seregeti boy wake kitandani,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

AMPOKONYA SIMU, AWAPIGA PICHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, Nay baada ya kuwakuta wawili hao wakiwa katika hali ya taharuki katika chumba cha nyumba hiyo ambayo alimpangishia Siwema, alimpokonya simu mpenzi wake huyo na kuwapiga picha za ushahidi wawili hao kisha akamchukua mwanaye kurudi Dar.

SIWEMA ATOKA NA KANGA MOJA
“Siwema baada ya kuona Nay amempokonya simu, alikurupuka akiwa na kanga moja kisha kumfuata ili arejeshewe simu yake, Nay aligoma na kukwea teksi akamuacha Siwema akilalama,” kilidai chanzo hicho.

NAY MSTARABU?
“Kiukweli Nay ni mstarabu sana maana hakuonyesha hasira za aina yoyote pamoja na kwamba aliwafuma laivu, alitoka taratibu, hakufanya ugomvi wowote kama watu wengine wanavyofanya pindi wanapofumania,” kilizidi kudai chanzo chetu.

NAY AKWEA PIPA, ARUDI DAR
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Nay kufanikiwa kumuacha Siwema na jamaa yake, alikwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupanda ndege kurejea maskani kwake jijini Dar.
“Jamaa (Nay) hakutaka kuuweka usiku, alichokifanya ni kukwea pipa na kichanga chake hadi jijini Dar na kwenda kumkabidhi mama yake,” kilisema chanzo hicho.

Siwema.

NAY ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu baada ya kuzinyaka habari hizo, alimvutia ‘waya’ Nay ambapo alipopatikana na kusomewa mashtaka ya kwenda kumfumania mchumba wake, alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa undani lakini akadai amemchukua mwanaye mikononi mwa Siwema kutokana na mchumba wake huyo kuzidiwa na mambo yake.

“Sitaki kuzungumzia chochote kwa sababu sitaki kuonekana mbaya, ila kiukweli nilienda Mwanza na kumchukua mwanangu na hapa ninapozungumza na wewe, mwanangu yupo chini ya uangalizi wa mama yangu mzazi,” alisema Nay.

SIWEMA KAFUATA SIMU YAKE
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, chanzo kilicho karibu na wawili hao kilipenyeza ubuyu kuwa Siwema ameibuka jijini Dar kwa lengo la kufuata simu yake ikidaiwa kwamba eti ina siri zake nyingi.

SIWEMA HAPATIKANI
Jitihada za kumpata Siwema kupitia simu yake ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa mikononi mwa Nay, jitihada zinaendelea ili na yeye afunguke ukweli wa tukio hilo.

TUJIKUMBUSHE
Nay na Siwema wamedumu kwenye uhusiano kwa takriban miaka mitatu ambapo wamefanikiwa kupata mtoto huyo mmoja. Awali, Nay aliwahi kuingia kwenye mgogoro na kigogo mmoja ambaye alikuwa akimtaka mrembo huyo lakini alifanikiwa kumuweka mikononi mwake kabla ya kumfumania na serengeti boy.

Soma Zaidi»

Zingatia Sana Haya Mambo Matano Unapokuwa Kwenye "Intavyuu"

0 comments
Kwenye nafasi nyingi za kazi siku hizi tunakutana na vitu na mambo mengi. Kazi nyingi zinatangazwa kisiasa lakini zinakuwa na watu tayari. Lakini hapa nataka kuzungumzia kazi ambazo bado hazina mikono ya watu sana. pensive woman biting lips Hivyo watu wengi huenda kwenye usaili wakihofu sana wenzao waliotangulia au watakaofuata watafanyaje, wasiwasi huo mara nyingine unaweza ukaathiri namna ambavyo utafanya usaili huo. Hutakiwa kuwa na wasiwasi wa vitu ambavyo huna uwezo navyo au hauna maamuzi navyo fanya yanayokuhusu na mambo mengine yataendelea. Fikiria kufanya vizuri kwenye usaili wako kwa kujua siri hii: 1. Zingatia Uwezo wako wa kipekee Kila mtu anatakiwa kuwa na ujuzi fulani wa kipekee na huo ndio ujasiri utakaokuingiza kwenye usaili bila wasiwasi. Je uwezo wako binafsi katika ujuzi huo uko wapi, labda ni mzuri katika utafutaji wa masoko, au mauzo na onyesha mifano ya vitu ambavyo umeweza kuvifanya. 2. Toa mifano halisi inayojulikana Watu wengi wana CV ambazo hazina vitu vya msingi ndani yake hivyo mwajiri anakuwa haoni kama ni mtu anayestahili nafasi fulani. Ili kuepusha hilo hakikisha CV yako imeshiba vitu halisi ambavyo umefanya hapo nyuma au kwenye kazi yako ya sasa. Hivyo vitu vinatakiwa kuwiana na kazi unayoomba! 3. Uwe na ushahidi unaobeba mifano yako katika maandishi Mahesabu au majeduari yanaweza kuonyesha namna gani ujuzi wako unafanya kazi na una weredi wa kiasi gani. Je uliongeza mapato, uliweza kupunguza matumizi au uliokoa muda kwenye kazi liyopita? Je uliweza kupata wateja wangapi kwenye kazi iliyopita kwa mwaka? au Mauzo yako yalikuwaje kwenye kitengo chako? 4. Onyesha kwa vitendo ujuzi wako Watu huajiri watu wanaowapenda. Wakati wa usaili unahitaji kuonyesha uwezo wako wa kuwasiliana vizuri. Je! unahusiana vipi na watu? Je wewe ni muadilifu na vinginevyo unavyohitaji kuonyesha! 5. Sahau ushindani, fanya yanayokuhusu Ili kuondokana na ushindani usiokuwa na sababu achana na kuwa na wasiwasi na watu wengine. Huhitaji msongo wa mawazo mwingine wakati wa kutafuta kazi, ila fikiria utaleta mchango gani kwenye kampuni unayoiendea.

Soma Zaidi»

Matonya Atupwa Jela Miaka 30 Baada Ya Kumbaka Mwanafunzi!

0 comments
Mfanyakazi wa ndani, Joseph Matonya (26) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mwanagati mwenye umri wa miaka 14.

Akisoma hukumu hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Hakimu John Msafiri alisema kuwa mshitakiwa huyo atatumikia adhabu ya viboko ambavyo atachapwa sita akiingia na sita akitoka.

Pia alisema Matonya atatakiwa kulipa fidia ya Sh milioni moja baada ya kumaliza kifungo hicho.

Hakimu Msafiri alisema mshtakiwa alitiwa hatiani baada ya upande wa mashitaka kuthibitisha mashitaka yake bila ya kuacha shaka kwa kuwa na mashahidi wanne na PF3 iliyothibitisha kubakwa kwa mwanafunzi huyo.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda alidai kwamba mshtakiwa apewe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.

Kabla ya hukumu, mshitakiwa huyo alidai kuwa yeye ni mgeni wa Mahakama na kwamba familia yake inamtegemea na kudai kuwa hakumbaka mtoto huyo.

Pia alidai kuwa adhabu hiyo imemuathiri kisaikolojia na kimwili na kwamba hatasahau maishani mwake.

Ilidaiwa kati ya Novemba na Desemba, 2013, maeneo ya Kitunda Mwanagati, wilayani Ilala, Matonya alimbaka mtoto wa miaka 14 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mwanagati.

Soma Zaidi»

UGOMVI KATI YA LIL WAYNE NA CASH BADO HAUJAISHA.CHEKI HII

0 comments
 weezy-cage-coco
Kampeni kubwa anayofanya Lil Waye ‘Free Weezy’ yakujitoa kwenye mkataba mkubwa wa cash money records chini ya Birdman inaendelea. Lil Wayne ametoa video ya wimbo kutoka kwenye mixtape yake ya Sorry 4 the Wait 2.   
Wezzy amefanya video akiwa ndani ya chumba chene umbo la jela na machuma yakimzunguka kuonyesha amefungiwa ndani ya record lebel ya cash money.
Mashairi kwenye huu wimbo yanasema
“Cash Money is an army, I’m a one-man army / And if them n**as comin’ for me, I’m goin’ out like Tony / Now I don’t want no problems, I just want my money, “All I got is Young Money, no more Cash, ni**a“.

Soma Zaidi»

Baada ya miaka 6,mahakama imeamua hivi kuhusu kesi ya Chris Brown.

0 comments
296-19Ap4r.St.55
Mpaka mwanzoni mwa mwaka huu ilikuwa imekamilika miaka sita toka Chris Brown aanza kutumikia kifungo cha nje kwa kosa na kumpiga na kumjeruhi aliyekuwa mpenzi wake, msanii wa rnb Rihanna.  Mahakama iliyokuwa ilisimamia kesi hio imetoa maamuzi mapya kuhusu kesi hio baada ya Chris Brown kumaliza kipindi chake cha majaribio ya kuishi bila kuvunja sheria.
Mahakama imesema kesi imeisha na msanii Chris brown ni mtu huru kwa asilimia mia moja. Chris Brown alifahamisha watu wake kwa kutwit
“IM OFF PROBATION!!!!!!!! Thank the Lord!!!!!!”
cb 4

Soma Zaidi»

HII NI KUTHIBITISHA KUWA BIFU BADO HALIJAISHA KATI YA YG NA DJ MUSTARD

0 comments
dj-mustard-austin-sxsw
Producer maarufu Dj Mustard amefanyiwa mahojiano hivi karibuni kuhusu muziki wake na wasanii anaowakubali kwenye rap na mtangazaji Steve Lobel.
Dj Mustard amesema “kwa maproducer anamkubali zaidi Dr Dre sababu ya sikio lake bora la muziki, producer mwingine ni Lil Jon kwa kuturusha kwenye club, bila kusahau Pharrell na Timbaland kazi zao zina mchango mkubwa kwangu” .
Dj Mustard amezungumza kuhusu msanii wa rap anayemkubali na kusema sio mshkaji wake YG, Ila ni rapa Drake wa Young Money.

Soma Zaidi»

HII NDIO LAANA YA PESA....CHEKI MJENGO MPYA WA DIAMOND ,UKIWA NA CHOO CHA THAMANI YA M.70

0 comments
d 000
Tumekuwa tukiona nyumba za mastaa wa nje ambazo huwa na vitu vingi vya kifahari kama mabwawa ya kuogelea, tv kwenye choo na mabafu na hata jikoni. Hii ni nyumba ya msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz iliyopo Dar es salaam maeneo ya Tegeta. Leo ametuonyesha Jiko, Sehemu ya kuogelea, na sehemu tofauti kwenye nyumba hio.
d 1 d 2 d 3 d 4 d 5 d 6 d 7 d 8 d 9 d 10 d 11 d 12

Soma Zaidi»

MCHAKATO WA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS ZAZINDULIWA RASMI LEO

0 comments
Kikao cha waandishi wa habari na waandaji wa tuzo za Kilimanjaro 2015, Nikatika uzinduzi wa mchakato wa tuzo hizi mwaka huu. Kwenye kupiga kura kwa sasa uteweza kufanya kupitia mitandao ya simu, website, Sms na Whatsup. Upigaji kura kuchagua washindi utaanza 1 May 2015.
Tuzo zitatolewa 13,6,2015
IMG-20150323-WA0002 IMG-20150323-WA0003 IMG-20150323-WA0004 IMG-20150323-WA0006 IMG-20150323-WA0007


CREDIT: SAMMISAGO.COM

Soma Zaidi»

Video:Nuhu Mziwanda Afunguka Makubwa Kuhusu Kupigwa na Shilole Pia Kutokujua Lugha ya Kingereza

0 comments

Kwa mara ya Kwanza, Nuhu Mziwanda amefunguka  mambo  kibao  ya  chumbani  baada  ya  kufanyiwa  mahojiano  ya  kina  na  Udaku  Tv .

Tazama  Video  hapo  chini  umsikie  alivyolizungumzia  suala  la  kunaswa  vibao  na  Shilole  pamoja  na  changamoto  za  lugha  ya  kiingereza.

Soma Zaidi»

MPYA KUTOKA KWA FID Q

0 comments

Mwanamuziki wa Hip Hop Farid Kubanda Fid Q,amesema tuzo aliyoipata ni mwanzo wa mafanikio katika Tasnia ya Muziki

Fid Q alisema hayo mara baada ya kupata Tuzo ya European Development of Tanzania mwaka 2015,kutokana na mchango wake kwa jamii

Akizungumza na Pro 24 alisema ataendelea kupigana ili kuhakikisha unapata mafanikio nje ya nchi

Alisema kuwa nyimbo zake zimekuwa zikifanya vyema sokoni ndani na nje ya nchi kutokana na mashairi mazuri

Fid Q alisikika akisema ''Ni faraja kubwa kwangu kupata tuzo hii maana nyimbo zangu zimekubalika nje ya nchi kimsingi nitaendelea kujituma kwa kuwa lengo langu ni kuitangaza nchi na kupata mafanikio zaidi alisema Fid Q

Soma Zaidi»